Jibu la hili swala limezua utata. Swala la usalama na usiri wa mwelekeo wa mtu wa kijinsia unatatanisha sanasana kwa wanaoishi kwenye nchi ambazo ushoga na usagaji zimepigwa marufuku. Iwepo usalama wa habari kati ya daktari na mgojwa haulindwi na sheria, basi itakuwa ngumu kuelezea daktari mwelekeo wako wa kijinsia.
Lakini, japo tutaweza kushirikiana na wahudumu wetu wa afya, basi wataweza kutuangalia vyema zaidi. Zungumuza nao kuhusu mwelekeo wako wa kijinsia na njia za ngono unazoshiriki ili waweze kukulinda ki afya kwa njia inayofaa zaidi.
Kumbuka ya kwamba ni haki yako kuhudumiwa na daktari ambaye anakuhakikishia usalama wako bila aibu. Iwepo daktari atakujulisha ya kwamba mwelekeo wako wa kijinsia sio sahihi, tafadhali mjulishe ya kwamba ungependa kuzungumzia maswala ya matibabu peke yake.
Tazama hii video yenye muda wa dakika moja kutoka Greater Than AIDS ndio upate kujua zaidi. (Ambatanisha na lugha chanzo ya kiingereza)